Kikao cha Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilicho chini ya Mwenyekiti wake Alfred Tibaigana, kilichokuwa kifanyike
kesho (Aprili 14) cha kujadili rufani ya Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, iliyowasilisha rufani ya kupinga kunyang’anywa
pointi tatu kwa kumchezesha Nadir Haroub 'Canavaro' katika mechi dhidi ya Coastal Union
kimeahirishwa.
Kamati hiyo
chini ya uenyekiti wa Kamishna mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana sasa
, kinatarajia kufanyika siku ya Jumanne (Aprili 17 mwaka huu) kuanzia mida ya saa 9 alasiri kwenye ofisi za TFF.
No comments:
Post a Comment