Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka
Uganda kuchezesha mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan itakayofanyika Aprili 21
mwaka huu.
Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni ni Brian Miiro. Waamuzi wasaidizi ni Mark
Ssonko na Lee Patabali wakati mwamuzi wa mezani ni Denis Batte.
Ejigu Ashenafi wa Ethiopia ndiye ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi hiyo
namba 15. Kamishna na waamuzi hao watawasili nchini Aprili 19 mwaka huu kwa
ndege za Ethiopian Airlines na Air Uganda.
No comments:
Post a Comment