Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Dennis Massue, kutoka Kituo cha Utafiti
Amani Tanga kuhusu vipimo vinavyofanywa na kituo hicho kwa kupima ufanisi na
ubora wa Viuatilifu vinavyoua Mbu katika Vyandarua kwa kutumia kifaa cha kupima
ubora ‘Cone Bioassay’, wakati alipotembelea katika maonyesho ya wanasayansi
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya
Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR) alipofungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa
sayansi ulioanza jana, jijini Arusha. Wa pili (kushoto) ni mke wa
Makamu, Mama Zakhia Bilal, (katikati) ni Dkt. Mwele Malecela.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma
hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti
wa Magonjwa ya Binadam (NIMR), ulioanza jana,jijini Arusha.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo.
Makamu pia alitoa zawadi kwa baadhi ya wadau washiriki wa mkutano huo walioweza kufanya vizuri katika tafiti zao.
Makamu pia alitoa zawadi kwa baadhi ya wadau washiriki wa mkutano huo walioweza kufanya vizuri katika tafiti zao.
Makamu
wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na wadau wa Sayansi
waliohudhuria mkutano huo wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi jijini Arusha jana.
No comments:
Post a Comment