Habari za Punde

*WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR WAPEWA SOMO KUHUSU MADHARA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA

 Profesa Chris Peter Maina wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akielezea na kufafanua umuhimu wa Mahakama, akitolea mfano ya ICTR kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kijamii katika kuhakikisha haki inatendeka, haswa katika matukio kama ya uhalifu wa kivita, wakati wa Kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakisikiliza Lecture ya Profesa Chris Peter Maina wakati wa mjadala wawazi wa kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Mwaka 1994.
 Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Stella Vuzo, akisoma hotuba kwa niaba ya Mshauri Mwandamizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda, ambapo amehimiza nchi washiriki kuwa na imani na mahakama ya ICTR.
 Mmoja kati ya wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
Mwanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
***************************
Na.Mwandishi wetu.

Wananchi wa Rwanda na Afrika Mashariki kwa Ujumla wametakiwa kulinda na kudumisha amani katika eneo la maziwa makuu kwa kuwa hiyo ndio misingi ya umoja amani na maendeleo.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Msemaji na Mshauri Mwandamizi wa Kisheria wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda Bw. Roland Amoussouga, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vizo, amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda inasikitika na inatoa pole kwa wale walioathiririwa na vita vilivyotokea mwaka 1994na kuwa iko pamoja nao.

Aidha amesema tunapaswa kuweka kumbukumbu ya waliopoteza maisha na walionusurika , ambao kwa sasa wameathirika kimwili na kiakili.
Katika kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.