Habari za Punde

*BFT, LOWASA WAMPONGEZA BONDIA SELEMAN KIDUNDA KUTEULIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA OLYMPIC


KATIBU wa shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini BFT Makore Mashaga pamoja na makocha na viongozi wa BFT kwa pamoja wamempongeza bondia Selemani kidunda kwa kuteuliwa kushiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajia kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza katika afla hiyo ya kumpongeza na kumtia moyo kuendelea na mazoezi kwa ajili ya michunano ya olipiki inayokuja karibuni aidha Makamu mwenyeki wa BFT Michael Changalawe amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa kwa kumpatia Kidunda Dola 100 walipokutana naye nchini  Dubai wakati wakirejea Tanzania.

Kambi ya ngumi inaingia kambini kesho tarehe 10 katika uwanja wa ndani wa taifa kwa ajili ya mazoezi zaidi mbali na mashindano hayo timu hiyo imeomba wafadhili wajitokeze kwa ajili ya kuipa sapoti ambapo wanatarajia kwenda botswana kwa ajili ya kuweka kambi ya bondia Kidunda na wengine kupima Viwango vyao.

Alisema Makore timu inakabiliwa na uaba wa wafadhili hivyo kuwaomba watu binafsi mashirika pamoja na makampuni kujitokeza kusaidia mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele nchini kwa kutoa sapoti moja kwa moja kupitia mchezo wa ngumi kwa sasa kambi hiyo itakuwa na mabondia kumi kila uzito


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.