Mintanga akiwa katika Mahakama Kuu leo alipofika kusikiliza kesi yake Picha na Mama Pipiro Blog. |
MAHAKAMA Kuu yaTanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), Shaabani Mintanga, Juni 11 mwaka huu.
Mahakama hiyo itasikiliza ushahidi wa upande wa Serikali wa kesi hiyo ya Mintanga ya kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8.
Kwa mujibu wa shajala ya Mahakama, kesi hiyo itaendelea kusikilizwa siku hiyo mbele ya Jaji Dkt. Fauz Twaib, ambaye alikuwa akisikiliza kesi hiyo tangu ilipofikishwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo iko katika hatua ya kusikilizwa mashahidi wa upande wa Jamhuri, ambapo mashahidi ambao wameshatoa ushahidi ni pamoja na Godfrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) , Charles Ulaya na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya ngumi, Nassor Michael.
Mintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2008, akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kg 4.8.
No comments:
Post a Comment