Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipera, Anthony Karoli (wapili kushoto) akiwa katika moja ya shunguli za kijiji jana.
Na Mwandishi wetu, Mvomero.
KATIKA kuhakikisha viongozi wa Serikali wanawajibika na wanakua waadilifu katika utekelezaji wa shughuli zao kwa jamii ipasavyo, Halmashauri ya Kijiji cha Kipera Kata ya Mlali Wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wamemtimua Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Fedinand Makunga kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ubadhilifu.
Viongozi hao wa Kijiji walikutana mapema wiki hii chini ya Mwenyekiti Anthon Karolin a wakiwa katika mkutano wao wa kawaida wa Halmashauri hiyo ya kijiji iiliibuka Agenda ya kumkataa Mtendaji huyo na kumtaka akibidhi ofisi mara moja, kutokana na shutuma mbalimbali za kiutendaji dhidhi yake.
Habari zilizoifikia blogu hii kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho walidai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na kuona utendaji mbovu wa Mtendaji huyo.
“Kiukweli huyu Mtedaji huyu hatufai na hatumtaki tena kijijini kwetu, maana amekuwa kero na kwa uongozi wa kijiji na matokeo yake wananchi wanaulala mikia uongozi wetu kuwa haufanyi kazi lakini kumbe anetukwamisha ni mtedaji wa Kijiji,” alisema mmoja wa wajumbe.
Mjumbe huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai kuwa miongoni mwa mambo ambayo anashutumiwa mtendaji huyo ni pamoja na uaminifu, kutokuleta maendeleo kijijini, na kuto tatua migogoro ya wananchi.
“Mtendaji amekuwa si mwaminifu maana amekuwa akipokea fedha kwa wananchi za michango lakini hazifikishi sehemu husika, na akiulizwa anakana kupokea fedha hizo ilhali mtoaji anathibitisha kumpatia,” alisema mjumbe Mwingine.
Pia Mtendaji Makunga, anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa mwekezaji wa Kizungu wa sghamba la kinyenze ili asishughulikie tatizo la mgogoro wa ardhi kijijini hapo na badala yake kuwaambia wananchi kama wanataka kushughulikiwa kwa mgogoro huo wachange Shilingi hamsini elfu.
Pia inadaiwa kuwa miradi ya maendeleo iliyopo kijijini hapo ya Ujenzi wa soko na kiwanda cha kusindika nyanya na matunda ambavyo vilianza ujenzi wake na Afisa Mtendaji aliyefariki, hayati Ramadhan Maguo hajaviendeleza kwa zaidi ya miaka 3 sasa na akiulizwa anadai kuwa Kipera sio kijiji chake na hakuja hapo kuleta maendeleo.
Mbali na shutuma hizo pia Mtendaji huyo anadaiwa kuruhusu kuwekwa kwa geti la ukusanyaji ushuru kijijini hapo ambapo wananchi hata wakipita na mazao yao ya shambani yakwenda kula hutakiwa kulipa ushuru na ushuru huo hauna manufaa kwa kijiji kwakuwa unaenda halmashauri na Kijiji hakipati hata senti.
Inadaiwa kuwa Mtendaji huyo alipotakiwa kuachia ngazi na kurudi kwa mwajiri wake na si kijijini hapo, alidai mbele ya baraza hilo la kijiji kuwa Kijiji hakina mamlaka ya kumfukuza hapo isipokuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero pekee.
Hata hivyo Viongozi hao ambao walichachamaa na kumtaka aondoke aende kwa huyo mwajiri wake na si Kipera maana mvomero ina vijiji vingi.
Kufuatia hatua hiyo wananchi wa Kipera wameupongeza uongozi wa kijiji chao na kuwataka wazidi kuwa wakali kwa viongozi ambao hawafanyi kazi zao na wamekuwa ni mzigo kwa kijiji.
No comments:
Post a Comment