Na Mwandishi Wetu, Jijini Dar
KIINGILIO cha chini 
katika mechi ya wapinzani wa jadi, Simba na Yanga keshokutwa Uwanja wa Taifa, 
Dar es Salaam kitakuwa Sh. 5,000 na kwa vibosile wa ukweli, yaani VIP A itakuwa 
ni Sh. 30,000- huko unashuhudia mechi kwa raha zote.
Timu hizo 
zinatarajiwa kukwaana kwenye Uwanja wa taifa katika moja ya mchezo wa funga dimba 
la ligi hiyo itakayofikia tamati hiyo keshokutwa.
Akizungumza na 
mtandao huu, ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba kikosi cha 
timu hiyo kitatua leo kwa ndege maalum kutoka Visiwani Zanzibar kilipokwenda 
kujiandaa na mchezo huo.
Alisema wachezaji 
wote wapo katika hali nzuri na wameapa kucheza kufa kupona kuhakikisha 
wanashinda mchezo huo ambao kama mambo yakienda vema watatangaza ubingwa wa 
msimu wa 2011/2012.
“Kikosi chetu chote 
kipo fiti na vijana watakuja kwa ndege maalum na kisha wataelekea 
katika hoteli moja ya kitalii kwa ajili ya kusubiria mchezo wetu na 
Yanga,”alisema.
Kwa upande wa Yanga 
kupitia kwa msemaji wao Louis Sendeu, kikosi cha timu hiyo kilichopo Bagamoyo 
mkoani Pwani kipo katika hali nzuri wakiendfelea na maandalizi ya  mchezo huo, huku 
viongozi wakiwajenga zaidi kisaikolojia.
Hata hivyo Sendeu 
alishindwa kuweka wazi ni lini timu yao itarejea jijini Dar es Salaam na kusema 
kuwa Bagamoyo na Dar es Salaam hakuna umbali mkubwa hivyo timu itarejea siku 
yoyote.
Katika hatua 
nyingine, kiingilio cha chini katika mchezo huo kinatarajiwa kuwa sh.5,000 kwa 
watakaokaa jukwaa la kijani bluu, wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi 
40,000 kitakachohusisha mashabiki watakaokaa jukwaa la VIP A.
Mashabiki 
watakaokaa VIPB watalipa sh.30,000, VIP B shilingi 20,000 huku watakaokaa jukwaa 
la orange watalipa shilingi 10,000.

No comments:
Post a Comment