Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, muda mchache uliopita ametangaza Baraza jipya la Mawaziri na kumteua, Dkt. Fenella 
Mukangara, kuwa Waziri wa Habari Utamadunia na Michezo, huku aliyekuwa 
Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akihamishiwa Wizara ya Mambo ya 
Ndani.
Akitangaza Baraza 
jipya la Mawaziri muda mchache uliopita Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete, aliwataja Mawaziri wengine kuwa ni Dkt. Amosa Makala, ambaye amemteua kuwa Naibu Waziri wa Habari Utamadunia na 
Michezo. 
Wengine ni Samuel Sitta 
anayeendelea kuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Shamsi Vuai Nahodha anakuwa Waziri 
wa Ulinzi, John Magufuli anaendelea na Wizara ya Ujenzi, Dkt. Mwinyi anakuwa Waziri wa Wizara 
ya Afya na Ustawi wa Jamii, Shukuru Kawambwa anaendelea na Wizara yake kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya 
Ufundi Stadi, Sophia Simba anaendelea katika wizara yake na Chikawe anarudi 
Wizara ya Katiba na Sheria.
Mathayo anaendelea 
na Wizara yake kama ilivyo kwa Mbawala na Tibaijuka, Chiza anakuwa Waziri wa 
Kilimo, Chakula na Ushirika, Maghembe anakuwa Waziri wa Maji, Mwakyembe anakuwa 
Waziri wa Uchukuzi, Kagasheki ana kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kigoda Wizara ya 
Viwanda, Mgimwa anakuwa Waziri wa Fedha, Mark Mwandosya Waziri asiyekuwa na 
Wizara Maalum. 
Endelea kuwa karibu na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com ili kupata majina mengine ya Baraza jipya yaliyotangazwa

No comments:
Post a Comment