Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA CHUO KIPYA CHA UFUNDI STADI VETA CHA MKOA WA MANYARA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi wa Korea Kusini, Young Hoon Kim, kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakati wa hafla ya ufunguzi wa chuo hicho iliyofanyika jana, mkoani Manyara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano:- wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo kipya cha VETA, baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichojengwa Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara. Hafla ya ufunguzi wa Chuo hicho ilifanyika , mkoani Manyara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa ufundi wa Magari wa Chuo kipya cha VETA cha Mkoani Manyara, Treekta dogo linalotumika kulimia na kupandia Mbegu za mazao, wakati aliokuwa akitembelea na kukagua majengo mapya ya Karakana ya chuo hicho baada ya kukifungua rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na viongozi wa Chuo cha Veta na viongozi wa Serikali baada ya ufunguzi rasmi wa chuo hicho uliofanyika, mkoani Manyara. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.