Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU NNE WA KUBADILISHANA UZOEFU BAINA YA SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA KUHUSU MAFUNZO YA ULINZI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. akisoma hotuba yake wakati akifungua mkutano wa siku nne wa kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi. Ufunguzi huo umefanyika leo,  katika Chuo kipya cha Jeshi National Defence College (NDC) kilichojengwa na Wachina eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. akisoma hotuba.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati Makamu wa Rais Dkt Bilal, akifungua mkutano huo leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Liutenant General wa Jeshi la Bangladesh, M F Akbar, baada ya kufungua rasmi mkutano wa siku nne wa  kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Meja General Charles Lawrence Makakala, baada ya kufungua rasmi mkutano wa siku nne wa  kubadilishana uzoefu baina ya Serikali ya Tanzania na China, kuhusu mafunzo ya Ulinzi. Ufunguzi huo umefanyika leo , katika Chuo kipya cha Jeshi National Defence College (NDC) kilichojengwa na Wachina eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakati akiondoka katika Chuo cha Mafunzo ya Jesho cha National Defence College (NDC). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kuufungua rasmi leo.
Wasanii wa kundi la JWTZ wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.