Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA JUKWAA LA UCHUMI WA KIJANI LA SIKU 3 MKOANI IRINGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa.
 Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, (wa pili kushoto) Eng. Ngosi C. Mwihava, akiwa ukumbini hapo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kijani.
 Sehemu ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, Linda Manu, wakati wa hafla ya uzinduzi huo leo.
 Msanii wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto, akighani maneno yake yenye ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani Iringa leo.
 Mrisho Mpoto (kulia) na mwimbaji wa bendi yake ya Mjomba Band, Ismail, wakiimba mbele ya meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani Iringa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, Leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.