Habari za Punde

*MAONYESO YA WAJASILIAMALI KUADHIMISHA SIKU YA AFRIKA YAFANA MNAZI MMOJA DAR LEO

 Adelina Aloyce ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya ADE FASHION Designer (katikati) akiwaonyesha moja ya nguo zake wateja waliofika katika banda lake katika maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Charity Food Products ya Mwanza  Sophia Kagose (kushoto ) akionyesha mifuko ya dagaa waliokaagwa njinsi walivyo sindikwa kwa utalaam katika maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa kampuni hiyo Favour Dietrich.
 Mkurugenzi wa Equator Natural Cosmetics Mrs Liwa (kushoto)  akiwaonyesha wateja wake waliofika katika banda lake jinsi ya kutumia Lotion ya kitanzania inayojulikana kwa jina Sanda Luwood, ambayo inatumika kwa kulainisha ngozi vizuri katika maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya Designer Glass Beads, Febronia Mihuwa, akimuonyesha  Tula Mkemwa jinsi ya kumechisha shanga ya shingoni na mkoba wakati alipotembelea katika banda lake katika maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.