Habari za Punde

*TANZANIA YAFANIKIWA KUPUNGUZA WAGONJWA WA MALALE

 NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

TANZANIA imefanikiwa kupunguza idadi ya watu wanaougua  ugonjwa  wa Malale  kutoka wagonjwa 380 mwaka 1996   hadi kufikia wagonjwa wawili katika kipindi cha mwaka jana.

Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ,Dk. Geoffrey Kiangi  kwa niaba ya  Mganga Mkuu wa Serikali katika semina ya siku moja ya kuwajengea  uelewa  waandishi wa habari juu ya ugonjwa wa Malale iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kinga na Tiba wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) jijiini Dares Salaam.


“ Haya ni mafanikio makubwa katika jitihada hizi kutokomeza mbung’o na Malale na kuufanya kuwa ni historia katika nchi yetu,” alisema Dk. Kiangi.


Aliongeza kuwa anapenda kuwapongeza   wadau wote  kwa mafanikio yaliyoptaikana na serikali  kwa kuwapatia wafugaji dawa za ruzuku za uogeshaji wa mifugo mabazo  zimechangia kuua mbung,o katika maeneo mengi ya wafugaji.

Dk. Kiangi aliwataja wadau hao kuwa ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara  ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizaraya Maliasili na Utalii(TANAPA), Shirikala Afya la Dunia(WHO) na Umoja wa Afrika katika mpango wake wa Kutokomeza Mbung’o na  Ndorobo  uitwao “Pan African TseTse and  Trypanosomias Eradication Campaign”(PATTEC).

 Aliyataja maeneo yanayoathiriwa na ugonjwa huo kuwa ni Tabora, Rukwa, Kigoma, Mara,  Arusha, Mbeya na Manyara, kwa upande wa wanyama huitwa Nagana na umesambaa katika mikoa yote  husababisha hasara  kubwa katika ukuaji wa uchumi na kipato cha familia na umekuwa ukiathiri watu wa kipato cha chini na wanaoishi katika maeneo ya vijijini karibu na misitu.

Dk. Kiangi alisema Tanzania imeathirika na wadudu aina ya mbung’o kwa asilimia 65 na kufanya watu milioni nne na mifugo milioni saba kuwa katika hatari ya kupata  ugonjwa  wa Malale(binadamu ) na Nagana(wanyama).

Alisema mfano wafugaji nchini  hupoteza takribani sh. Bilioni 12.7 kwa mwaka   kutokana na mifugo yao kufa na kupunguza uzalishaji wa maziwa na bidhaa zinazotokana na mifugo.

Naye Mtaalamu mwingine kutoka wizara hiyo , Charles Mwalimu alitoa wito kwa wataalamu wa afya kufanya uchunguzi wa damu kwa  ajili  kutambua  vimelea vya  ugonjwa wa    malale wakati wanapopiima wa kutambua ugonjwa  wa  ugonjwa wa malaria ili kuiwezesha Tanzania  kufanikiwa kutokomeza ugonjwa wa  huo na kupunguza athari zake.

Alizitaja baadhi ya athari hizo kuwa ni kifo, kupungua kwa nguvu kazi, kiuchumi , kupungua kwa watalii,kuathirika kwa mfumo wa fahamu , kuvunjika kwa ndoa na unyanyapaa.

 Aliwataka wananchi kufika katika vituo vya afya ili kuweza kupata tiba mapema ili kupunguza athari zake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.