Habari za Punde

TAMASHA LA KARIAKOO FESTIVAL LAZINDULIWA DAR NMB WAISHIKA KARIAKOO

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Alex Mgeni (kulia), wakati alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wafanyabiashara Kariakoo ‘Kariakoo Festival’. lililoanza jana Agosti 17/2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, 
Tamasha hilo lililodhaminiwa na Benki ya NMB, linaendelea kwa muda wa wiki moja katika viwanja hivyo huku likishirikisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali. Wa pili kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio na Mwenyekiti wa Wafanyabishara wa Kariakoo, Martin Mbwana.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila (kushoto), akizungumza jambo na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, wakati alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wafanyabiashara Kariakoo ‘Kariakoo Festival’. lililoanza  jana Agosti 17/2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Tamasha hilo lililodhaminiwa na Benki ya NMB, linaendelea kwa muda wa wiki moja katika viwanja hivyo huku likishirikisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Tamasha la Kariakoo Festival, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya  NMB baada ya kutembelea katika Banda la benki hiyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Alex Mgeni (kulia), na Mwenyekiti wa Wafanyabishara wa Kariakoo, Martin Mbwana. (katikai) wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini dar es Salaam, leo kwa ajili ya kufungua rasmi Tamasha la Kariakoo festival lililodhaminiwa na Benki ya NMB.
DAY TWO...................
Ofisa wa Bank ya NMB Tawi la Bank House, Fortunatus Chacha (kulia) akimfafanulia jambo mteja wakati akihakiki Kadi ya Benki ya mteja huyo alipotembelea katika Banda la NMB kwenye maonesho ya Kariakoo Festival yaliyodhaminiwa na benki hiyo, yanayoendelea kwenye Viwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Venda wa Bank ya NMB (kushoto) akimsajili mteja wake ili kumfungulia Akaunti ya Benki hiyo wakati walipokuwa katika zoezi maalum la kutoa huduma katika kituo cha Daladala cha Karume jijini Dar es Salaam, leo.
Venda wa Bank ya NMB (kulia) akimsajili mteja wake ili kumfungulia Akaunti ya Benki hiyo wakati walipokuwa katika zoezi maalum la kutoa huduma katika kituo cha Daladala cha Karume jijini Dar es Salaam, leo.
Venda wa Bank ya NMB (kushoto) akimpiga picha ya Passport size mteja wake kwa ajili ya msajili na kumfungulia Akaunti ya Benki hiyo wakati walipokuwa katika zoezi maalum la kutoa huduma katika kituo cha Daladala cha Karume jijini Dar es Salaam, leo.

Ofisa wa Benki ya NMB, Brenda Magina, akitoa elimu kwa mteja wake aliyetembelea katika Banda hilo ili kupata ufafanuzi kuhusu changamoto za akaunti yake. benki ya NMB inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki katika maeonesho ya Kariakoo Festival yaliyodhaminiwa na benki hiyo yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
fisa wa Benki ya NMB, Paul John, kutoka Tawi la NMB Bandarini akimsajili mteja wake aliyetembelea katika Banda hilo kwene maonesho ya Tamasha la Kariakoo Festival yaliyodhaminiwa na NMB yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Benki ya NMB, Paul John, kutoka Tawi la Bandarini, akimpiga picha mteja wake ili kumfungulia Akaunti ya Benki, wakati wa Tamasha la Kariakoo Festival lililodhamniniwa na NMB, linaloendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Ofisa wa Benki ya NMB, Moreen David, akitoa elimu kwa mteja wake aliyetembelea katika Banda hilo ili kupata ufafanuzi kuhusu changamoto za akaunti yake. benki ya NMB inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki katika maeonesho ya Kariakoo Festival yaliyodhaminiwa na benki hiyo yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.