Habari za Punde

NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 125, VITI NA MEZA VYA MILIONI 20 KWA SHULE ZA MSINGI KARAKATA NA BANGULA

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, akikata utepe kama ishala ya kupokea msaada wa Madawati 125, Viti 25 na meza zake kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege,Restus Assenga wa pili (kushoto) kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa Shule za Msingi Karakata na Bangula, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara (Kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bangula, John Sendeu na wa pili (kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Karakata, Maria Shayo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, (aliyekaa) akifurahia baada ya kupokea msaada wa Madawati 125, Viti 25 na meza zake kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege,Restus Assenga wa kwanza Wa pili (kushoto) kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa Shule za Msingi Karakata na Bangula, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024. Wa tatu (kulia waliosimama) ni Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara (Kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bangula, John Sendeu na wa (pili kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Karakata, Maria Shayo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, akipeana mkono na Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga, kama ishala ya kupokea msaada wa Madawati 125, Viti 25 na meza zake kutoka Benki ya NMB, kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa Shule za Msingi Karakata na Bangula, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara.
Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, akiwakabidhi zawadi ya shukrani Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga (wa pili kushoto) na Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara, baada ya kukabidhi msaada wa madawati, Meza na Viti vyake kutoka kwa  wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024.  
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, akifurahi pamoja na baadhi ya wanafunzi Queen Andrea (kulia) na Halima Yusuph, baada ya kupokea zawadi ya Madawati 125, Viti na Meza zake kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga (wa kwanza kushoto waliosimama)  wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024.  Katikati waliosimama nyuma ni Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara, (kulia) ni Mwalimu MKuu wa Shule ya Msingi Bangula, John Sendeu na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Karakata, Maria Shayo
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, akipokea zawadi ya shukrani kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bangula, John Sendeu, baada ya kupoea msaada wa madawati, Meza na Viti vyake kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga (wa pili kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024. Wa pili (kulia) ni Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala Mkuu, Flora Mgonja, akiwakabidhi zawadi ya shukrani Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga (wa pili kushoto) na Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara, baada ya kukabidhi msaada wa madawati, Meza na Viti vyake kutoka kwa  wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh, milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam leo Juni 19 2024.  
Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Afisa Tawala Mkuu Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
**************************
KATIKA kutekeleza Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Benki ya NMB imekabidhi msaada wa madawati 125, viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya Sh. Mil. 20 kwa ajili ya wanafunzi na walimu wa Shule za Msingi Karakata na Bangulo, Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Shule ya Msingi Karakata, Kata ya Kipawa, ambako Meneja wa NMB Tawi la Airport, Restus Assenga, alikabidhi msaada huo kwa Afisa Tawala Mkuu, Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja, naye kuwakabidhi walimu wakuu wa shule hizo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Assenga alisema changamoto za Sekta ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya benki yake, ambayo hutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi ya kila mwaka, kusaidia utatuzi wake, kama inavyofanya katika Afya na Majanga.
“Tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kufanikisha utoaji elimu bora na bure mijini na vijijini, nasi kama wadau tunajiona tunao wajibu wa kuunga mkono hilo, ndio maana NMB hutenga asilimia moja ya faida yetu kurejesha kwa jamii.
“Msukumo wa kufanya hivyo unatokana na ukweli kuwa jamii ndio iliyowezesha NMB kuwa hapa ilipo, inapoongoza sekta ya fedha kimafanikio, vifaa hivi tunavyokabidhi leo ni ushiriki wetu kuhakikisha jamii inayotuzunguka inanufaika na faida tunayopata,” alisema Assenga.
“Tunajisikia fahari kupokea maombi mbalimbali ya kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu na afya, na mwaka huu peke yake NMB imetenga zaidi ya Sh. Bil. 5 za kusaidia nyanja hizo na leo tuko hapa kutoa madawati 125, viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya Sh. Mil. 20 kwa shule hizi mbili,” alisema Assenga.
Baada ya kupokea msaada huo kwa Assenga, Afisa Tawala Mkuu Wilaya ya Ilala, Bi. Flora Mgonja alikabidhi viti, meza na madawati hayo kwa Walimu Wakuu wa Shule ya Msingi Karakata, Maria Shayo na Shule ya Msingi Bangulo, John Sendeu.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa, kabla naye kukabidhi kwa Walimu Wakuu wa Shule ya Msingi Karakata, Maria Shayo na Shule ya Msingi Bangulo, John Sendeu, Bi. Flora aliishukuru NMB aliyoitaja kama kinara wa utatuzi wa changamoto za Elimu na Afya sio tu wilayani Ilala, bali wilaya na mikoa yote Tanzania.
“Serikali inafanya juhudi kubwa katika kuboresha mazingira ya Sekta ya Elimu, lakini bado inahitaji sapoti ya wadau kama hivi wafanyavyo NMB, ambao leo wanaenda kutoa madawati ya kuketisha wanafunzi takribani 400 na walimu 50.
“Madawati 125, viti 50 na meza 50 sio msaada mdogo, ni mkubwa sana, wanamuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake, kutoka moyoni kabisa tunasema ahsante sana kwa kuwawekea wanufaika hawa mazingira rafiki ya kutoa na kupata elimu.
“Wito wangu kwa walimu na wanafunzi ni kutunza misaada hii, ili siku moja NMB watapokuja hapa kusaidia utatuzi wa changamoto nyingine, wakute vifaa hivi bado vinatumika,” alisema Bi. Flora huku akiwataka wazazi kushirikiana na walimu katika kulea kimaadili watoto.
Awali katika usomaji wa risala ya shule zote mbili kwa mpigo, Bi. Maria Shayo (Mkuu wa Shule ya Karakata), alisema shule zote mbili zinakabiliwa na changamoto mbalimbali na kuitaka Benki ya NMB kutowachoka watapopokea maombi mapya.
“Shule ya Karakata iliyoanzishwa mwaka 1979 yenye wanafunzi 1,350, inakabiliwa na upungufu wa matundu ya choo 15, changamoto ambayo iko pia katika Shule ya Msingi Bangulo iliyoanzishwa mwaka 2002, yenye wanafunzi 3,224 inayohitaji matundu 100 ya choo.
“Wito wetu kwa NMB ambayo ni baba rasmi wa shule zetu hizi ni kuendelea kutusaidia ujenzi wa chumba maalum na kompyuta angalau 40, ili kuwezesha wanafunzi wetu kujifunza na kurahisisha utendaji kazi wa walimu,” ilisema sehemu ya risala hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.