Habari za Punde

*MAWAZIRI WA ARDHI, MAZINGIRA WATOA TAARIFA YA ZOEZI LA BOMOA BOMOA NYUMBA ZA UFUKWENI NCHINI


Katika picha kutoka (kushoto) ni Katibu wa Wizara ya Ardhi, Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, baada ya mazungumzo hayo.

*Tibaijuka, Huvisa wapewa meno kuanza zoezi la Bomoa Bomoa Nyumba za ufukweni.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la Bomoa bomoa  nyumba zilizojengwa maeneo ua Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.