Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen (wa pili kulia) akizungumza na kupongeza mafanikio katika kupanua elimu ya sekondari nchini na kusema kwamba mpango wa kuwa na angalau shule moja ya sekondari katika kila kata umefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Pia amepongeza mafanikio katika kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wanajiunga na masomo ya sekondari na kumekuwa na usawa wa kijinsia katika uandishikaji wanafunzi shule za msingi.
Msaidizi Mshauri wa Umoja wa Mataifa Bw. Tobias Rahm, akitoa majumuisho katika mkutano wa taasisi za Umoja wa Mataifa na Jukwaa la Wahariri. Rahm alisema kwamba anamatumaini kuwa vyombo vya habari vitaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi katika kuongea ufanisi na uelewa wa shughuli zao.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment