Waziri wa Ujenzi Dkt., John Magufuli (mbele) akikagua upanuzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta jana jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa DSM Mwantumu Mahiza, na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango (mwenyetai) Picha na Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO.
Sehemu ya ujenzi wa baadhi ya ujenzi wa daraja eneo la Bonde la Kawe Mbezi Tangi Bovu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wa
DART jijini Dar es Dar es salam kwa Waziri wa
Uchukuzi Dkt. John Magufuli (kushoto) . Mradi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa
jijijni.
*********************************
*********************************
NA MAGRETH KINABO –MAELEZO
WAZIRI wa Ujenzi , Dk. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya mabasi 29 kutoka Kimara hadi Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha .
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Magufuli leo(jana) wakati alipotembelea miradi hiyo miwili ili kungalia shughuli za ujenzi ambapo alifurahishwa na kazi hizo huku akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.
“Mkandarasi unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kabla ya wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie sisi serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.
Waziri Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) na Mamlaka ya (DAWASA) kuondoa miundombinu yao haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi wa DART.
Waziri wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya Jangwani na Ubungo, ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa na ujenzi mwingine wa vituo utagharimu jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia.
Awali Meneja wa mradi , Frank Rohde kutoka kampuni hiyo , alisema changamoto inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi huo kutoka bandarini ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.
Akizungumzia kuhusu tatizo hilo Waziri Magufuli alisema atazungumza na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo vitolewe haraka.
Aidha Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike ya Japan kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12 inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na kuacha kusingizio cha mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.
“Mvua zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna nchi mvua inayesha muda mrefu kuliko Tanzania na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na hiyo sababu ninyi nchi za nje mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha. Ni lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko la muda wala mtaji,” alisisitiza.
Wakati huohuo Waziri Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe kwa kuwa sharia ni msumeno.
“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.
Akizungumzia kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa DART Cosmas Takule alisema utatengeneza ajira 80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo utakamilika katika kipindi cha miezi 36.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam , Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.
No comments:
Post a Comment