Mshambuliaji wa timu ya Soka ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’, Mwanahamisi Omari akichuana kuwania mpira na beki wa Ethiopia, Tiruanchi Mengesh, wakati wa mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Ethiopia ilishinda 1-0. Kwa matokeo hayo sasa Twiga Stars itakuwa imetolewa katika mashindano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mwanahamisi, akiruka kwanja la beki wa Ethiopia.
Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamis Omari 'Gaucho' akimtoka beki wa Ethiopia, Berktawet Girma
Wachezaji wa Ethiopia, wakishangilia ushindi wao baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Asha Rashid 'Mwalala' akitoka uwanjani huku akiwa na huzuni baada ya timu yake kulala kwa bao 1-0.
Kocha Mkuu wa Twiga Stars akiwa ameduwaa baada ya kumalizika kwa mchezo. Picha zote na Habari Mseto.
No comments:
Post a Comment