Habari za Punde

*JAKATE MWEGELO AENDESHA MNADA WA KONDOO WA AMANI KUPINGA KUNDI LA UAMSHO LA ZANZIBAR

Mbunifu wa Mitindo nchini, Jakate Mwegelo (wa tatu kushoto) akiendesha mnada wa Kondoo wa Amani, katika mnada maalum.

Na Mwandishi Wetu
Mbunifu wa mitindo nchini, Jokate Mwegelo juzi aliendesha mnada wa Kondoo wa amani maalum kupinga matukio ya kuhatarisha amani yaliyotokea Zanzibar hivi karibuni.
Mnada huo uliandaliwa na wanamichezo kikundi cha Taifa cha Jogging kwa kushirikiana na wageni wao wa kundi kutoka  Zanzibar lijulikanalo kwa jina la Kitambi Noma.
Mbali ya kufanya mazoezi, wanamichezo hao walikusanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja chini ya mgeni Rasmi, Kanali Mstaafu na mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Idd Kipingu ambaye aliwapongeza waandaaji wa shughuli hiyo kwa kuhamasisha amani nchini.

Kipingu alisema kuwa amani ndiyo silaha pekee kwa sekta zote pamoja na michezo kwani kutokuwepo kwake hakuna kitakaochofanyika katika jamii.
Alisema kuwa kilichofanyika kwa wanamichezo hao ni mfano wa kuigwa na kuwataka wanamichezo nchini kupigania amani mbali ya kushiriki katika michezo tofauti.
Katika Mnada huo, Jokate ambaye kwa sasa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ubinifu wa mitindi ya Kidoti aliweza kumuuza kondoo huyo kwa sh. 200,000 kutoka kwa wanamichezo hao.

Mrembo huyo wa zamani alisema kuwa baada ya kumuuza kondoo huyo, aliondoka na kundi la Kitambi Noma na kwenda Zanzibar ambako atachinjwa na kuliwa kama ishara ya kudumisha amani.
“Nimefarijika sana kwa kushiriki katika mnada huu, mwaliko wangu umetokana na jinsi gani ninavyojishughulisha katika masuala mbali mbali ya Jamii, mbali ya mitindo au kama mmoja wa warembo waliofanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania,” alisema.
Baadhi ya wanamichezo wanaounda kikundi cha Kitambi Noma kutoka mjini Unguja.

1 comment:

  1. achana na UAMSHO MALAYA WEWE. UMEKIUZA EEEEE UMEAMUAKUTAFUTA UMAARUFU KWA UAMSHO . TUTAKUCHINJA....................

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.