Habari za Punde

*MAXIMO KUTUA NCHINI KURITHI MIKOBA YA PAPIC- YANGA

Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo, anatarajia kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya kutua Klabu ya Yanga na kuchukua mikoba ya Kocha anayemaliza muda wake katika Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeelezwa.

Kocha huyo anatarajia kuwasili nchini akiwa na Kocha msaidizi wa Viungo, huku akiwa ameongozana na mkewe kutokana na kuwa nashughuli pevu ya kukiandaa kikosi hicho cha Yanga kinachotarajia kushiriki michuano ya Kombe la Kagame.

Aidha imeelezwa kuwa mara tu baada ya kupokea maombi ya kukinoa kikosi hicho Maximo hakuwa na pingamizi lolote bali alikubaliana na maombi hayo moja kwa moja huku akitoa mapendekezo ya kuwasajili wachezaji awatakao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Katika mapendekezo hayo ya wachezaji aliowahitaji Maximo ni pamoja na Beki wa Simba, ambaye hadi sasa bado anazua gumzo na mtafaruku mkubwa baina ya Klabu hizo mbili za watani wa jadi Simba na Yanga, Kelvin Yondan, pamoja na Kipa Ali Mustapha 'Bartez'.

Chanzo cha habari hizi kutoka Klabu hiyo ya Jangwani kimetonya kuwa baadhi ya wachezaji wengine waliokwishamwaga wino katika Klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na, Beki wa timu ya Kagera Sugar, David Luhende, mchezaji anayecheza soka la kulipwa na timu ya DC Motema Pembe, Mussa Hassan Mgosi, Owen Kasule, kutoka Klabu ya Hoang Anh Gia Lai, ya Vientnam, Middie Kagere,  kutoka timu ya Polisi Rwanda na mchezaji wa Tanzania, anayecheza Soka la kulipwa nchini Canada, Nizar Khalfan, pamoja na Said Bahanuzi na Juma Abdul kutoka timu ya Mtibwa Sugar.

Aidha imeelezwa kuwa Kipa huyo anayehitajika na Kocha mpya Maximo, 'Bartez' tayari amekwisha saini mktaba na Klabu hiyo, huku Kipa namba tatu wa timu hiyo, Shaban Kado, akiachiwa kwa Mkopo kurejea katika kikosi cha timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.