Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika, akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma   leo asubuhi, baada ya kukataa kufuta kauli yake ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, 'eti' ni dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea. Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma
*******************************
Akizungumza na baadhi ya wanahabari waliohitaji kujua hatima yake baada ya kutolewa nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati Kikao hichi kikiendelea, Mnyika alisema kuwa atatoa tamko rasmi 
kuhusu tukio hilo huku akisisitiza kwa kuendelea kutoa kauli yake kuwa,''kwa ufupi ubovu 
wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini mpango wa Taifa 
wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi,tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. 
Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza analoliongoza,pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita  ni matokeo pia ya udhaifuwa Taasisi ya Rais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. 
Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. 
Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho'' alimaliza kusema Mnyika.
Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho'' alimaliza kusema Mnyika.
.jpg)
No comments:
Post a Comment