Habari za Punde

*MWANAUME AOTA MATITI BAADA YA KUTUMIA ARV'S, AIOMBA SERIKALI NA WADAU KUMSAIDIA AWEZE KUTIBIWA


Khamis, akiwaonyesha Waandishi wa habari za UKIMWI, (AJAT) jinsi alivyoota Matiti.
KATIKA hali isiyo kuwa ya kawaida, Mkazi wa kijiji cha Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Khamisi Tanga (46) ameota matiti.

Imedaiwa kuwa, Khamis, ameota matiti hayo baada ya kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi   ARV’S.
     
Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda Wilayani humo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAT),Khamisi (Pichani) alisema alipatwa na mkasa huo miaka mitatu iliyopita.

Akisimulia namna alivyoanza kuugua alisema awali aliona matiti yake yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini hakujua kama lingeweza kuja kuwa tatizo kubwa kama lilivyo sasa.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki anayohudhuri na kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa imesababishwa na dawa anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo na kupewa aina nyingine.

Hata hivyo Khamisi, alisema kwamba pamoja na kubadilishiwa dozi hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na kuongeza kwamba hivi karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile ambazo zilimsabishia matatizo hayo, na tayari ameanza kupatwa na maamuvu aliyokuwa akisikia awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.

Kwa mujibu wa Khamisi, ''Nimeshahangaika sana kupata matibabu hadi Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, lakini hadi leo sijapatiwa tiba stahili ya kunitibu tatizo hili, Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yeyote ili niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha hasa mbele ya wanaume wenzangu''.alisema Khamis

Aidha Khamis, alisema kuwa tayari amekwisha pima kansa na matiti lakini bado hadi leo Matiti yanaendelea kukua na kuuma sana hasa wakati anapolala.

Pia alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kumsaidia ili arudi katika hali yake 
ya uanaume kwa kuwa maisha kwa sasa kwake yamezidi kuwa magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na hali hiyo.

Kwa upande wa mtaalam wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU, kuwa ni jambo la kawaida japo hutofautiana.

Dk. Komakoma alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na kusema kuwa Tatizo hilo la Khamis,  sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa dawa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.