Habari za Punde

*MCHEZASINEMA MAARUFU KUTOKA MAREKANI, DEIDRE LORENZ KUKIMBIA MBIO ZA MT. KILI MARATHON


Mcheza sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazotarajia kuanza kutimua vumbi Juni 24,mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi. 

Mbio hizi zilizoanzishwa na Mama Marie France, kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani, mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 Continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.

Ujio wa mcheza sinema huyo aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight,  na nyingine nyingi, unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. 

Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani, lakini akahamia katika jiji la New York City linalojulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.

Deidre Lorenz, ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombea tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. 

Mcheza sinema huyo  ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini, Juni 21, kukimbia mbio hizo ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. 

Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka jana.

Naye mwanzilishi wa mbio hizo Mama Marie Frances, ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. 

Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon,  nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt, matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.

Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri. 

Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.

Mount Kilimanjaro Marathon, zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa za kilometa 42. 

Pia kutakuwa na mbio za akilometa 21, kilometa 10 na kilometa 5 kwa watoto. 

Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kushiriki kukimbia mbio hizo.

Imetolewa na;
Grace Soka
Afisa  Uhusiano wa Mt. Kilimanjaro Marathon

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.