Habari za Punde

*MIKAKATI NA UTEKELEZAJI IMARA NDIYO SIRI YA USAFI WA MKOA WA KILIMANJARO

Mkoa wa Kilimanjaro ndiyo Mkoa unaoongoza kwa usafi wa mazingira nchini, na hasa kutokana na mazingira safi yasiyokuwa na uchafu unaotokana na wananchi wa mji huo. 
Imeelezwa kuwa siri ya kuwa na mji msafi na wenye sifa lukuki kwa usafi ni mikakati inayowekwa na Mkoa na utekelezaji wake tofauti na mikoa mingine ambayo imetawaliwa na longolongo, ikiwa ni pamoja na Mgambo wanaowasumbua wananchi wafanyabishara kwa kuwakamata na kisha kuwaomba rushwa ama kuondoka na bidhaa zao ili kuwaachia na kutoawatoza faini kama ilivyoagizwa. 
Kwa upande wa jiji la Dar es Salaam ambalo ni sura ya Nchi kumekuwa na mipango lukuki iliyokwisha wekwa siku za nyuma ya kutokomeza uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuwakamata wanaoonekana wakichafua mazingira ama kutupa taka hovyo ama kukojoa hovyo, lakini hii imeonekana ni tofauti kwani mara kadhaa wamekuwa wakiripotiwa Mgambo wa Jiji na Polisi Jamii, wakiwakamata raia na kisha kuwaachia baada ya kuwaomba kitu kidogo 'Money Pesa', Je ni lini Jiji la Dar es Salaam litafikia hatua kama iliyofikiwa na Mkoa wa Kilimanjaro?? 
Kwa mji wa Kilimanjaro kila anayekamatwa hata kwa kutupa kipisi cha Sigara hulipa faini ya Sh. elfu 50, bila huruma, nasi pia inabidi tufikie huko ili kuwakomesha hata abiria wanaokunywa maji akiwa katika daladala na kisha akatupa chupa popote tu bila kujali kuwa anachafua mazingira.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.