Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wanaotarajia kushiriki shindano la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 , siku ya jumamosi, wanatarajia kutembelea makumbusho ya Taifa ikiwa ni ziara maalum ya mafunzo.
Shindano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, jijini Dar es Salaam , mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia warembo hao katika harakati zao za kielimu.
Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
“ Kama ndani ya Jumba la Makumbusho, kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika duniani,”alisema.
Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaedelea vizuri, ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa, Sufianimafoto na Full Shangwe.
No comments:
Post a Comment