Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba, akizindua mradi wa uvunaji maji ya mvua uliopo Hospitali ya Wilaya ya Iringa katika mtaa wa Frelimo mjini Iringa jana. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni 50 na unatarajia kuwanufaisha wakazi zaidi ya 100,000 wa maeneo hayo. Kutoka (kushoto) ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu, V Mushi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba, akimshukuru Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda kwa kampuni yake kufadhili mradi huo muhimu wa maji Hospitalini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba, akimtwisha ndoo ya Maji Augusta Mtemi, mmoja kati ya wakazi wa maeneo hayo aliyefika kushuhudia uzinduzi huo.
Tanki litakalo tumika kusambaza maji katika mradi huo.
Hii ndio Hopspitali ya Frelimo iliyopo Manipaa ya Iringa ambayo itafaidika na mradi huo.
No comments:
Post a Comment