Mshambuliaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Ivory Coast katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kutinga katika fainali ya kombe la dunia 2014, mchezo uliochezwa jana usiku. Katika mchezo huo Mshambuliaji wa Chelsea Solomon Kalou, ndiye aliyeanza kuibomoa ngome ya Stars kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza, na msumali wa pili na mwisho ukipigiliwa na mshambuliaji pia wa Chelsea ya Uingereza Didie Drogbana. Kwa matokeo hayo sasa Stars inatakiwa ushindi wa zaidi ya magoli matatu kwa bila katika mchezo wake wa marudiano utakaochezwa hapa nyumbani katika uwanja wa Taifa.
CRDB YARAHISISHA UPATIKANAJI WA MIKOPO KWA WAFUGAJI
-
Wafugaji nchini wameendelea kunufaika na huduma za kifedha baada ya
kuongezeka kwa uelewa wao kuhusu masuala ya fedha na uwekezaji, hatua
iliyowezesha ku...
14 hours ago
No comments:
Post a Comment