Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti aina ya Mroliondo katika eneo la Chem chem ya Maji Njoro,leo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Terezya Huvisa, akishiriki zoezi la upandaji miti katika eneo hilo baada ya Makamu kuzindua rasmi zoezi hilo leo mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha BEP-Environmental Initiatives Consortium, Jensen Siria, kuhusu matumizi na utengezaji wa majiko ya gharama nafuu, wakati alipotembelea katika Banda la kikundi hicho katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyozinduliwa Kitaifa na Makamu wa Rais, leo Viwanja vya Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa Kundi la Mradi wa i WASH, Kelvin Mwanshilo, wa Shirika la Care, kuhusu vyoo mbadala vya Gharama nafuu, wakati alipotembelea katika Banda la kikundi hicho katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyozinduliwa Kitaifa na Makamu wa Rais, leo Viwanja vya Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mche wa zao la Kahawa wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipokuwa akizindua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika Viwanja vya Mashujaa Mkoani Kilimanjaro.
Kikundi cha ngoma za asili cha mkoani Kilimanjaro kikitoa burudani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoani Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ambayo yanafanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment