Wananchi wajiji la Washngton Dc pamoja na Watanzania wakiwa katika viwanja vya Down Town jana Jumamosi katika kuitikia wito wa kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya maziwa, utafiti na elimu dhidi ya ugonjwa huo. Maradhi ya saratani ya maziwa yanakisiwa kuwadhuru watu 25 milioni kote ulimwenguni ambapo kama hatua haitochukuliwa inakisiwa watu milioni 10 kufa katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Tukio hili liliaza kwa matembezi ya vikundi vya mataifa mbali mbali wanaoishi katika Jiji hilo la Washngton
Dc nchini marekani.
Sehemu ya Watembeaji wengi waliohudhuria katika matembezi hayo kutoka majimbo mbali mbali nchini Marekani.
Rais wa Jumuia ya waTanzania DMV Mh. Iddi Sandaly, wa kwanza (kushoto), Waheeda Margaret Gathesha, Chief wa swahilivilla Abou Shatry, Aunt Rehema, pamoja na Salma Jay Jay pia walikuwepo katika matembezi hayo ya kupigana na ujongwa wa saratani ya maziwa Washington DC.
Wazawa wa kitanzania wanaoishi nchini Marekani, wakiwa katika matembezi ya kupiga vita ogonjwa wa saratani ya maziwa mapema jana ndani ya washington D.C nchini marekani.
Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo & amp; Mitazamo ya wengine. Mchango wako katika kazi yoyote ulenge kujenga jamii yenye Kujitambua, Kujithamini na Kujiwajibisha, huu ndiyo ujumbe wa wanadada hawa.
Warembo wa kiTanzania wakiwa mstari wa mbele katika mpango mzima wa kutimiza hadhma hiyo.
Team Tanzania wakipata picha ya pamoja katika kuitikia wito wa kuunga mkono matembezi hayo.
Kina kaka nao pia hawakubaki nyuma kuunga mkono Susan G.Komen. kumaliza vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa Susan G.Komen. 2012! ndani ya Washington DC.
Latino Team pia hawakujiweka nyuma kupiga vita ungonywa huo hatari unaowapa tabu kina Mama.
Mamia ya wananchi wakiwa katika matembezi ya Susan G.Komen. 2012! Down Town Washington DC.
Dada Sofia akiwa katika matembezi pamoja na Team Tanzania na nyengine mchanganyiko.
Team Tanzania baada ya kumaliza matembezi ya Susan G.Komen. dhidi ya kupiga vita maradhi ya Saratani ya maziwa. Picha na swahilivilla.blogspot.com
No comments:
Post a Comment