Habari za Punde

*UN YAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

 Gertrude Lyatuu (kulia) kutoka Umoja wa Mataifa akizungumzia mfumo wa uwezeshaji utakaopelekea uzalishaji, usambazaji na matumizi ya bidhaa na huduma ikiwa ni matokeo ya kuboresha maisha ya mwanadamu kwa muda mrefu kwa kutunza mazingira bila kukiangamiza kizazi kijacho.
 Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi, akifafanua jambo kuhusu  Tanzania kama mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, ambapo  amesema Tanzania imeandaa  Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano huo mkuu wa mazingira utakaofanyika nchini Brazil hivi karibuni.

Bw. Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo sasa".

Aidha, Muyungi, ameongeza kusema kuwa Mkutano huu utaainisha hatua zitakazoangalia utekelezaji na kuhuisha nguzo zote tatu za maendeleo endelevu (mazingira Uchumi na Jamii) kwa kufuata  kanuni za usawa huku tukitambua  tofauti katika uwajibikaji na uwezo.

Upatikanaji wa njia mpya, za  ziada, thabiti, zinazotabirika za kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa nchi zinazoendelea.
Ofisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Stella Vuzo, pamoja na baadhi ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.