Na Mwandishi Wetu WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' kesho Jumatano, wanatarajiwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya kuanza safari ya kumpata mshindi wa shindano hilo litakalofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam. Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na wanachosubiri ni siku ya shindano ifike. Alisema kuwa kitongoji hicho kina warembo wenye sifa na wanaojiamini ambao wamepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke. Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho. "Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe mwenyewe," alisema mratibu huyo. Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Winnie Karaya. Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM. Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu. |
Tuzo za watendaji wakuu bora 100 wa mwaka
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Sharif Ali
Sharif amewataka vijana wa Kitanzania kubuni miradi inayoendana na sera za
uw...
7 hours ago
No comments:
Post a Comment