TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imeibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya The Express ya Uganda, katika mchezo wake wa kirafiki uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Mabao ya Yanga yamefungwa katika kipindi cha kwanza na yote yakiwekwa kimiani na Jerry Tegete, ambaye alimalizia kazi nzuri ya pasi nzuri za mwisho kutoka kwa mchezaji Said Bahanuz, aliyejiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar.
Yanga iliwakilishwa na wachezaji hawa katika kikosi cha kwanza:- Ally Mustafa 'Barthez', Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete, Nizar Khalfan, Kelvin Yondan, Nadir Cannavaro 'Canavaro', Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva.
No comments:
Post a Comment