Penati ya mwisho iliyopigwa na Athuman Idd 'Chuji', imeipeleka timu ya Yanga katika hatua ya Nusu Fainali katika michuano ya Kombe la Kagame, wakati wa mchezo wa Robo Fainali uliochezwa leo jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Yanga na Mafunzo. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1 huku Mafunzo ikiwa ya kwanza kuandika bao lake katika dakika ya 35. Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Mafunzo ilikuwa mbele kwa bao 1-0, baada ya kuanza kwa kipindi cha pili Dakika ya kwanza tu ya kipindi cha pili Said Bahanuzi, aliiandikia bao timu yake ya Yanga, bao ambalo lilidumu hadi kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo, jambo lililopelekea timu hizo kuingika hatua ya kupigiana mikwaju, ambapo Yanga ilifunga mabao yote huku Mafunzo wakikosa penati moja. Katika mchezo wa kwanza APR imeichapa URA mabao 2-1, na kesho Simba watakutana na Azam.
EWURA KANDA YA KASKAZINI YAWANOA VIONGOZI WA WILAYA YA KOROGWE
-
*Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kupitia Kanda ya
Kaskazini, leo tarehe 5 Machi 2026 imetoa elimu kwa viongozi wa Wilaya ya
Kor...
38 minutes ago

Simba wajue kutesa ni kwa zamu. Ninawatakia kila la kheri wavuke hatua hiyo ili ikiwezekana wakutane na yanga imara!!!!!
ReplyDeleteDirector matai.