Mabondia Alpjonce Joseph (Mchumiatumbo) na David Michael Mlope (Zola D – King) watapambana katika Tamasha la Watani wa jadi linalotarajia kufanyika katika Sikukuu ya Idd El Fitri kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari Temeke.
Pambano hilo ambalo limeandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania SHIWATA lina lengo la kukusanya fedha za Ujenzi wa nyumba za kisasa za gharama nafuu kwa ajili ya Wasanii, Waandishi wa Habari na Wanamichezo katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBC) ambalo inasimamia pambano hilo la Mabondia hawa watakaocheza katika uzani wa juu (Heavy weight) raundi nane (8) pia kutakuwa na pambano moja la utangulizi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango vya mabondia wa kulipwa wa TPBC, Boniface Wambura amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo wakati wa Sikukuu za Iddi el fitri, Agosti, 2012.
Mwenyekiti wa SHIWATA Cassim Taalib alisema pamoja na pambano hilo, kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga (Veteran) katika Uwanja huo huo wa Chuo cha Bandari Temeke na mshindi wa mchezo huo atazawadiwa ng’ombe dume.
Taalib alisema kwamba kikundi cha Mchiriku cha Jagwa kitatumbuiza, Roman Mg’ande wa Msondo atapigana mieleka na Lumole Matovolwa (Big na upande wa wanawake Sophia Lubuva wa Simba atapambana na Mwajuma Jimama wa Yanga huku washangiliaji wa Mpira Pesa (Simba) watapambana katika mpira wa miguu na Watani wao wa jadi Yanga Bomba.
Tamasha litapambwa na mechi ya Mpira wa Kikapu ya Ngongoti pamoja na mashindano ya Pikipiki ambayo yanatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watoto na wakubwa ambao siku hiyo watakuwa wakisherekea Sikukuu ya Idd el fitri baada ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani, Wasanii wa Bongo Flava nao watakuwepo.
No comments:
Post a Comment