Kocha mpya wa Klabu ya Yanga, Mbelgiji Thom Saintfiet, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana na kupokelewa mashabiki wa Klabu hiyo. Kocha huyo baada ya kuwasili anatarajia kusaini mkataba ramsi na Klabu hiyo, leo ambapo atakabidhiwa mikoba ya kujenga kikosi cha Yanga na kusimamia kikosi cha timu ya Vijana wa U 20 wa timu hiyo. Kocha huyo tayari amekwisha toa matumaini makubwa kwa wapenzi wa Klabu hiyo na wachezaji huku akisema kuwa kazi kubwa na ya kwanza ataanza kuandaa kikosi cha kutetea Ubingwa wa Kombe la Kagame katika michuano inayotarajia kuanza hivi karibuni.
RC TANGA AWATAKA WALIOPANGA KUCHOMA MATAIRI MKESHA WA MWAKA MPYA WASITHUBUTU
-
Na Oscar Assenga, TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amewataka wananchi wa mkoa
wa Tanga ambao wamepanga kutumia matairi kuchoma moto...
1 hour ago

No comments:
Post a Comment