Habari za Punde

*MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao  na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange akitoka kuweka silaha ya jadi kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
 Kutoka (kushoto) Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho....., Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq,  wakiwa katika viwanja vya Mnazi  Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
 Sehemu ya wageni waalikwa na Mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
 Askari wa Jeshi wakishiriki katika maadhimisho hayo, hapa wakiweka silaha begani.
 Ni ishara ya kutoa heshima kwa Mashujaa wapiganaji.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Huyu ni Mzee CUF, ni maarufu kwa upigaji picha za kuuza 'BANYAA' huyu pia ni miongoni mwa wapiganaji ambao walipata kupigania haki ya Mtanzania wa leo enzi hizo, ambaye kwa sasa kazi yake kubwa ni kujishughulisha na uuzaji wa picha katika shughuli mbalimbali, hapa akihaha kusaka matukio ya kuweka katika karatasi ya picha zake ambazo baadaye atafanya biashara. Mzee huyu baada ya kuona siku ya leo ni muhimu hata kwake pia lakini akiweka kazi yake mbele zaidi ili kujipatika kipato alionelea ni vyema naye pia akakumbukia mavazi yake haya aliyoyavaa na kutinga nayo eneo la tukio ili kuepuka kusumbuliwa na wahusika aweze kuingia kirahisi eneo la tukio kama unavyomuona akiwa bize na vazi lake huku akiwa na begi  kubwa la kamera wakati kajikamera alikonako ni kibiriti. Hii yote ni janja tu ilimradi mkono uende kimiani.
 Mzee CUF, akiwa bize kunasa picha za wajeda wakiwa katika paredi, begani ni bonge la begi la kamera  ambalo ndani yake halina kilichokusudwa.
 Mzee CUF bado yu bize........
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiomba dua kwa niaba ya waislam wakati wa maadhimisho hayo leo.
 Kiongozi wa dini ya kikristo, Mchungaji Kamoyo, akiomba sala kwa niaba ya wakristo wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati akiondoka kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo baada ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.