Habari za Punde

*SHINDANO LA MISS SINZA 2012 KUFANYIKA JULAI 13 WAREMBO WAPANIA KUFUNIKA

Warembo wa Redds Miss Sinza wakiwa katika pozi la picha la pamoja wakati wa mazoezi yao ya maandalizi ya shindano lao yanayoendelea katika ukumbi wa Mawela Social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na Hoteli ya Vatican chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma, ambaye anashikilia taji la Top Model . Warembo hao watapanda jukwaani Julai 13 mwaka huu kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika mashindano ya  Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania. Picha na Mpiga Picha wetu
**********************************************
JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza  kuwania taji la Mrembo bora wa Sinza “Redds Miss Sinza 2012” katika shindano linalotarajia kufanyika julai 13, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mawela Social (Ten Star  Lounge) uliopo karibu na Hotel ya Vatican City, Sinza, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtandao huu Mratibu wa shindano hilo, Majuto Omar, alisema kuwa warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma, ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model. Alisema kuwa mazoezi ya warembo hao yanafanyika kwenye ukumbi wa mashindano hayo, Mawela social kuanzia saa 8.30 mchana.

“Warembo wamepania kufanya kitu cha kihistoria siku ya mashindano na hii inatokana na ukweli kuwa wamejiandaa vilivyo na kwa sasa wanamalizia tu baadhi ya vitu vidogo vidogo vya mashindano hayo, alisema Majuto.

Alisema kuwa lengo kubwa la mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mbali ya taji la Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake  Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.

“Tuna warembo bomba na moto wa kuotea mbali ambao kwa sasa wameonyesha kupania kufanya kile ambacho kimesubiliwa na wadau fani ya urembo wa mitaa ya Sinza na vitongoji vyake, hii inatokana na ukweli kuwa mashindano haya ni ya mwisho kwa upande wa vitongoji jijini,” alisema.

Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment aliwataja warembo hao kuwa ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Esther Mussa, Christina Samwel, Nahma Said, Shadya Ali, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.