JUMLA ya wachezaji 11 wa timu ya Coast Union ya Jijini Tanga, wamemaliza mikataba yao ya kuichezea timu hiyo, inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na sasa wako huru kujiunga na klabu yoyote itakayowahitaji.
Kwa mujibu wa Klabu hiyo ya Coastal Union, wachezaji hao ni Ben Mwalala, Samwel Temu, Francis Busungu, Ahmed Shiboli, Lawrence Mugia, Daudi Chengula, Godfrey Mmasa, Mwinyi Abdulrahman, Sabri Ramadhan China, Soud Abdallah na Ramadhan Wasso.
Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment