Habari za Punde

*TIMU ZA AS VITA YA CONGO NA URA YA UGANDA KUTUA BONGO JULAI 12

 Kikosi cha timu ya AS Vita ya Congo (DRC).

TIMU  za AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na URA ya Uganda zinatarajia kuwasili nchini Julai 12 mwaka huu kushiriki michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 14 mwaka huu.

Wachezaji wa timu ya URA ya Uganda.
AS Vita Club ambayo iko kundi A pamoja na timu za Simba (Tanzania Bara), Ports (Djibouti) na URA itawasili saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikipitia Nairobi.


Nayo URA itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jioni ya siku hiyo kwa ndege ya Air Uganda. AS Vita imepangiwa kufikia hoteli ya Rombo Green View wakati URA itakuwa hoteli ya Royal Valentino.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.