Wakulima wanawake na wataalamu wa chakula kutoka Oxfam wakiangalia zao la muhogo, wakati walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wanawake katika kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani hivi karibuni. Wataalamu hawa wa chakula walikuwa nchini kwenye ziara ya mafunzo katika maswala ya lishe na mchango wa wakulima wanawake kwenye uzalishaji wa chakula.
Meneja Kampeni wa Oxfam, David Moriarty (kulia), akigawa fomu za kushiriki shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' kwa kina mama wa kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni mara baada ya kuzindua shindano hilo. Shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' linaratibiwa na Oxfam kutambuwa na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
Wakulima wanawake kutoka vikundi mbalimbali katika kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo wakipata futari baada ya kumalizika kwa mjadala wa hali halisi ya kilimo na uzalishaji wa chakula wilayani humo. Mjadala huu uliratibiwa na Oxfam na kuwahusisha wakulima wanawake kama mpango endelevu wa Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
No comments:
Post a Comment