Habari za Punde

*YANGA YAZINDUKA KAGAME YAICHAPA WAU MABAO 7-1, KIIZA SHUJAA

 Hamis Kiiza, akiwatoka mabeki wa timu ya Wau El Salam ya Sudan ya
 Kusini,  wakati wa mchezo wa kundi C, kombe la Kagame uliochezwa 
leo joni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga 
ilishinda mabao 7-1. Mvua hiyo ya mabao ya Yanga ilianza katika 
Dakika ya 12 kwa bao la kwanza na la pili dakika ya 17, yote 
yakifungwa na Said Bahanuzi, Hamis Kiiza, alifunga mabao manne 
katika dakika ya 19, 25 30 na 35 na bao la saba likiwekwa 
kimiani na Nizr Khalifan, katika dakika ya 85, huku bao la kufutia 
machozi la Wau likiwekwa kimiani na Khamis Deshama Ulama, 
katika dakika ya 90+1..
 Haruna Niyonzima, akifavya vitu vyake adimu.
 Hamis Kiiza, aking'ara kuwania mpira na beki wa Wau.
 Sehemu ya mashabiki, waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
 Athuman Idd 'Chuji', akichanja mbuga kukatika msitu wa mabeki.
 Niyonzima, akimhadaa beki wa Wau, hapa ilikuwa ni three by four.
 Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuph Manji, akizungumza na wachezaji katika Klabu yao Jangwani, leo kabla ya kuondoka kuelekea Uwanjani kwa ajili ya mchezo huo, na kuwapa moyo wachezaji na mzuka wa mchezo.
 Stephane Mwasika, akichuna na Nahodha wa Wau, Khamis Leon.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji (kulia) akizungumza na Kocha wa 
timu hiyo, wakati wa mapumziko baada ya kumalizika dakika 45 za 
kipindi cha kwanza uwanjani hapo.
Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akichuana na beki wa 
tmu ya Wau El Salam ya Sudan ya Kusini, Ismaul Mussa Juma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.