Habari za Punde

*KUMBUKUMBU YA MIAKA 2 YA MAREHEMU OMARY SAIDI ULEMBO, AGOSTI 12, 2012


Keshokutwa siku ya Jumapili ya Tarehe 12-Agosti-2012 utakuwa umetimiza miaka 2 sasa  tangu ulipotutoka  ghafla katika dunia hii. 

Ndugu yetu Omary Saidi Ulembo, ulituaga ukiwa mzima wakati unaelekea Nairobi Kenya kwa shughuli za kikazi, lakini umauti ulikukuta huko huko na kurejesha nyumbani ukiwa marehemu.

Sisi tulikupenda lakini Mola alikupenda zaidi. Mapenzi ya Allah Yatimizwe.
 
Unakumbukwa zaidi na Mama yako Bi. Husna Omary, Mke wako Sheila Omary, watoto wako, Harith na Shamim, Kaka zako, wadogo zako, dada zako, Fatuma, Mtumwa, Ziada, Mwanaasha, Lemna, Thureiya, Samira,  wadogo zako Ngabwe, Rama, Saidi, Shafy, Sadiki, Salim, Juma. na wengineo... Wajomba zako Shanni na Mbwana,
 
Mama zako akina Mama  Mwanaasha, Mama Yusuph, Mama Shamte, Mama Ponda, Mama Jongo, bila ya kusahau ndugu, jamaa na marafiki wa karibu, Ali Kirro, Pambwe, Khalfani, Abdalla na wengineo.
 
Tunamuomba Mwenyezi Mungu  ailaze roho yako mahali pema peponi.
AMIN...
 
 HIDAN .O. RICCO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.