Habari za Punde

*MISS TANZANIA JULIETH WILLIAM AIBUKIA TASNIA YA FILAM, AJA NA MPYA 'SISTER JULIET' YENYE KISA KAMA 'KIFO CHA KANUMBA'

 Miss Tanzania No. 3, 2009, Julieth William, nyota wa filamu mpya ya "Sister Julieth"
 Miss Tanzania No. 3, 2009, Julieth William (kushoto) na Sylvia Shally, Miss TZ No.4 2009 waliocheza filamu mpya ya "Sister Julieth", inayozungumzia kisa cha Kifo cha Kanumba.
**************************
MISS Tanzania Na.3 wa mwaka 2009, Julieth William, ametunga filam mpya inayokwenda kwa jina la Sister 'Julieth' na kumshirikisha mrembo mwenzake aliyemfuata katika nafasi ya 4, kwenye shindano la Miss Tanzania la mwaka 2009, Sylvia Shally.

Filamu hiyo ambayo iko katika hatua ya uhariri inaelezea kisa cha kijana ambaye anatuhumiwa kumuua rafikiye wa kike wakati

wakiwa peke yao chumbani na kesi mahakamani inamuelemea kijana huyo.

Sister Julieth, nafasi ambayo inachezwa na Sylvia, anakuja kama mzimu na kumtetea kijana huyo, ambaye anakumbana na

upinzani mkali kutoka kwa mawakili wa upande wa mashitaka.

Mrembo huyo aliyegeukia katika uigizaji, alisema hii ni filamu yake ya kwanza kucheza, kama ilivyo kwa Sylvia.

Alipohojiwa na mtandao huu kuhusiana na kisa cha Filam hiyo kuwa kama kina uhusiano wowote na tukio la fifo cha Staa wa Muvi aliyefariki hivi karibuni Stive Kanumba, kutokana na kuwa kisa cha filam hiyo kinafanana na tukio la kifo cha staa huyo ambaye hadi leo bado kesi yake inaunguruma Mahakamani, Juli alikana na kusema kuwa kisa cha filam hiyo ''Ni kisa tofauti kabisa, ni kisa kinachouhusisha mzimu unaokuja duniani kutoa ushahidi'' alisema Juli.

"Ni kati ya filamu za hisia kali. Iko katika hatua za mwisho za kuhaririwa na wakati wowote itatoka."

Alisema katika filamu hiyo amewashirikisha pia wasanii wengine maarufu akiwamo Dude.

Katika shindano la Miss Tanzania 2009 ambalo Julieth alishika Na.3, Miriam Gerald aliibuka mshindi wa kwanza, Beatrice

Lukindo alikuwa wa pili wakati nafasi ya nne ilishikwa na Sylvia na Sia Ndaskoi alikamilisha Top 5.

 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.