Habari za Punde

*NGASA AKABIDHIWA JEZI YA BANKA SIMBA KUTAMBILISHWA KWA MASHABIKI SIMBA DAY

Mchezaji mpya wa Simba, Mrisho Ngassa akikabidhiwa jezi yake No, 16, iliyokuwa ikitumiwa na Mohamed Banka, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Klabu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu,leo mchana.
*******************************
MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa rasmi jezi No,16 iliyokuwa ikitumiwa na mchezaji Mohamed Banka, ambaye pia alijiunga na timu hiyo akitokea Yanga kabla ya kutemwa katika msimu uliopita.

Ngasa sasa atakuwa akitumia jezi hiyo katika mechi za klabu yake mpya ya Simza msimu huu, wa ligi Kuu unaotarajia kunza hivi karibuni.

Amesema, Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.

Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.

"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu. 

Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, alikwa akiwahitaji sana" alisema.

Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia ya baba yake mzazi inajirudia, ambapo alikumbushia kuwa hata baba yake mzazi, Khlfan Ngassa, aliwahi kuichezea klabu ya Simba miaka ya 1990.

Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre Richard na James Kisaka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.