Habari za Punde

*NHIF YACHANGIA SH. MILIONI 3 UJENZI WA ZAHANATI YA SOMANGILA WILAYA YA TEMEKE DAR ES SALAAM


Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) , Mariam Wilmore (kulia) , akimkabidhi hundi yenye thamani ya sh. Milioni 3 Diwani wa Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila (wapili kushoto), wengine ni Meneja wa NHIF Kanda ya Temeke, Imelda Likoko, . Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Somangila Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila (wapili kulia), akionesha hundi ya sh. Milioni 3 aliyokabidhiwa na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mariam Wilmore (kulia) kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Somangila. Wengine ni Meneja wa NHIF Kanda ya Temeke, Imelda Likoko (wapili kushoto) , na Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Anjela Mziray.
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya Somangila, Wilaya ya Temeke, Aisha Mpanjila amesema kitendo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya cha kusaidia Zahanati ya Mbutu kitahamasisha wananchi wengine kuchangia ujenzi unaoendelea katika zahanati hiyo na hatimaye kumaliza tatizo la miundombinu.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, jana ulikabidhi hundi yenye thamani ya sh. Milioni 3, kwa lengo la kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama na watoto. 

Akipokea msaada huo, Diwani Mpanjila, alisema kuwa NHIF imeonesha njia na imekuwa mfano wa kuigwa hasa kwa kutambua mahitaji ya wananchi katika sekta ya afya.

“Kweli nyie ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya…pamoja na kusaidia wanachama wenu katika huduma za matibabu lakini mmekwenda mbali zaidi kwa kutoa hata msaada wa kuboresha vituo vya kutolea huduma msaada ambao unamgusa kila mtu…nawapongeza sana,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa maeneo hayo ambao ni wanufaika wa moja kwa moja na zahati hiyo kuunga mkono Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuchangia ili ujenzi wa wodi zilizopo zikamilike na zianze kutumika mara moja.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mariam Wilmore amesema NHIF imeguswa na matatizo ya wakazi wa kata hiyo hivyo itaendelae kusaidia kadiri ya uwezo wake.

Zahanati ya Mbutu inahudumiwa zaidi ya wakazi wa mitaa SITA inayozunguka kata hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.