Polisi wa nchini Afrika ya Kusini leo, wamewafyatulia risasi na kuwaua Waandamanaji 30, waliokuwa wafanyakazi wa Mgodi wa Platnum, wakati wakiandamana huko Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg, wakiwa wamebeba marungu na mapanga leo mchana.
Imeelezwa kuwa mmiliki wa Mgodi huo wa Platnum, Lonmin ndiyo hasa amekuwa chanzo cha vurugu za wafanyakazi hao kutokana na kudai malipo, uliochochewa na mvutano baina ya vyama viwili vya wafanyakazi.
Vurugu zilizokuwa zikiendelea wakati wa mgomo huo zilisha sababisha vifo vya watu 10 kabla ya leo.
Tukio hilo la polisi kumwaga damu za wananchi ni kubwa tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Waandamanaji hao wakiwa nje ya mgodi huo wakati wakiandamana na marungu na mapanga wakimtaka mwajiri wao kuwalipa malipo yao.
No comments:
Post a Comment