Habari za Punde

*RAIS KIKWETE ATEMBELEA MASHAMBA YA MANANASI,AONANA NA RAIS MPYA WA GHANA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha  Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra Ghana leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa  kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la   Bomarts Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam  nje kidogo ya jiji la Accra leo. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya  mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana, baada ya  kumtembelea na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra, jana  wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.