Matajiri walio wengi wanaomiliki magari yanayotoa huduma za kusafirisha abiria kama Daladala, huwa hawajui kama magari yao hutoa huduma kulingana na vibari vya ruti walivyokata, ambapo madereva wengi huzua ruti mpya kila wanapokuta abiria wengi wanaoelekea mahala fulani na hata ikiwa nje ya mkoa.
Na ili kufidia safari yenye ruti ndefu basi madereva na makondakta huwa wakifosi kubeba mizigo hata isiyoendana na aina ya gari kama inavyoonekana picha gari hili aina ya Hice likiwa limebeba mizigo juu na nyuma na Baiskeli pamoja na abiria ndani, huku bado kondakta akiendelea kuitia abiria.
No comments:
Post a Comment